IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Mpango wa  Kujifunza Qur'ani kwa njia ya intaneti Wazinduliwa na Urais wa Misikiti Miwili Mitakatifu

17:37 - January 16, 2024
Habari ID: 3478203
IQNA - Urais wa Haramain (misikiti miwili mitakatifu ya Makka na Madina) imezindua programu ya kujifunza Qur'ani Tukufu kwa njia ya intaneti.

Mpango huo unaoitwa Haramain, unalenga kuendeleza ufundishaji wa Qur'an Tukufu katika kiwango cha kimataifa.

Ofisi ya Urais Mkuu wa Haramain ilisema programu hiyo inatumia teknolojia ya kisasa zaidi kufundisha Qur'ani Tukufu.

Taarifa ya ofisi hiyo imeongeza kuwa wale wanaochukua kozi hizo wataweza kusahihisha usomaji wao, kupata umahiri wa Tajweed, na kuhifadhi Quran.

Kozi hizo zinatolewa kwa lugha sita, ambazo ni Kiarabu, Kiingereza, Kiurdu, Kiindonesia, Kimalei na Kihausa, kupitia apu ya Miqrat al-Haramain.

Watakaomaliza kozi hizo kwa mafanikio watatunukiwa vyeti pamoja na ruhusa au ijaza ya kuwa hafidh na qari rasmi kutoka kwa wataalamu wa fani ya mitindo kumi ya usomaji wa Qur'ani Tukufu.

3486824

Urais wa Haramain pia hutoa huduma tofauti kwa Mahujaji na waumini wanaotembelea Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume huko Madina .

Kati ya huduma hizo ni kusambaza Misahafu (nakala za Qur'ani Tukufu ) ikiwemo Misahafu maalumu ya  maandishi ya nukta nundu (Braille) kwa  watu wenye ulemavu wa macho.

captcha